Msanii wa BongoFleva, Diamond Platnumz ametua Marangu wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro na kuahidi kupanda mlima Kilimanjaro hadi kileleni, safari inayoanza leo.

Loading...
Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili wilayani humo, Diamond alisema safari hiyo itakayochukua takribani siku tano, alitamani kwenda siku moja na kurudi.

Hata hivyo, alisema kutokana na ushauri wa Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Dk Hamis Kigwangalla ambaye ndio mwenyeji katika kampeni ya 'Kili Challenge Twenzetu Kileleni" alimtaka aambatane na watu wengine zaidi ya 130 watakaopanda mpaka wote wafike sawa.

 "Mimi uwezo wa kupanda mlima siku moja ninao kwani ni sawa na shoo yangu moja, narudi nawaacha kina Mwana FA wakijikongoja," alisema Diamond.

Kwa upande, wake msanii MwanaFA, alisema pamoja na nchi kujaliwa vitu vizuri ambavyo havilipiwi kwa Mungu ukweli ni kwamba wasanii bado hawajafanya kazi yao ipasavyo.