Tanzania imefanikiwa kuvunja rekodi ya Uganda kwa tamasha la JAMAFEST kuhudhuriwa na watu wengi zaidi toka lilipozinduliwa jumapili iliyopita na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Loading...
”Mara nyingi nyakati za jioni watu wengi huwa kwenye tamasha wakishatoka makazini wanakuja kuburudika kwahiyo tumevunja rekodi tupo vizuri sana ”amesema Mbuya
Mbuya amesema sababu za wasanii wa bongo fleva kupewa nafasi ya kutumbuizwa katika tamasha hilo ikiwa ni moja ya mpango wa aina zote za sanaa zionekane.
Nedy atoa sababu za kuwavimbia Jux na Ruby
Tamasha hilo liliopambwa na wasanii wa kizazi kipya lilikuwa na mvuto wa aina yake katika burudani kutoka kwa wasanii kama Diamond Platnumz, aliyefanikiwa kutumbuizwa katika uzinduzi wa tamasha hilo wikendi iliyopita, huku wengine ni Barnaba Classic, Mario, Dj D Ommy, Jux, G Nako, Mboso, Maua sama, Navy Kenzo, Country boy na wengine wengi.
Mwaka 2017 tamasha hilo lilifanyika nchini Uganda ambapo watu zaidi ya 46,000 walishuhudia tamasha la tatu la jumuiya ya Afrika Mashariki la utamaduni ‘JAMAFEST’.
0 Comments