Maoni mgawanyiko yaliyotolewa kumuhus Robert Mugabe alipokuwa hai, hayabadilika hata baada ya mauti yake . Wazimbabwe wanakumbuka kuhusu ni nini alichowaachia kiongozi huyo aliyeiongoza Zimbabwe kwa miaka 37.
Wakitumia #RIPMugabe ama #LALAsalama baadhi wanamsifu ama shujaa, mtetezi wa hadi ya watu weusi, huku wengine wakisema alikuwa mkombozi aliyegeuka kuwa mkandamizaji . Wakili wa Zimbabwe , mwanaharakati na mkosoaji wa serikali ya chama cha Zanu-PF , Fadzayi Mahere, anatafakari maoni tofauti kumuhusu namna Bwana Mugabe atakavyokumbukwa
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @advocatemahere
Baadhi ya jumbe za Twitter zilizolenga namna Mugabe atakavyokumbukwa kwa uchumi wake ambao uliathiri kila sekta ya maisha , hususan huduma za matibabu
Loading...
Hospitali za umma zimetawaliwa na ufisadi pamoja na usimamizi mbaya , hali ambayo imesababisha utoaji wa huduma duni kwa wa wagonjwa.
Madaktari na wauguzi hufanya migomo ya mara kwa mara kuhusu mishahara .
Kwamba Bwana Mugabe - Mpigania haki za Waafrika aliyekuwa mstari wa mbele - mara kwa mara amekuwa akipata matibabu nchini Singapore na amefariki katika nchi ya kigeni ni kitu ambacho hakitasahaulika miongoni mwa wengi.
0 Comments