Ndugu yangu fahamu kuwa kuoa kuna faida nyingi mno, lakini hapa tutazitaja chache katika hizo ambazo ni :
- Ndoa ni sababu ya kubakia kizazi kikiendelea kuzaana hapa Duniani.
- Ndoa ni sababu ya kuhifadhi tupu ya mtu husika kutokana na zinaa,
- Ndoa ni sababu ya kuhifadhi macho kunako kutazama vitu vya haramu (Yaani Wanawake wasio halali yako).
- Ndoa ni sababu muhimu sana ya kuyaondoa maji yaliyojazana katika mwili wa mtu husika, maji hayo ni yenye madhara makubwa endapo yataendelea kuwepo mwilini, maji hayo si mengine ni manii.
- Ndoa ni sababu ya kuustarehesha moyo wako kwa ladha ambayo haielezeki kwa ufasaha wowote bali ladha ile nafsi pekee ndiyo inayoifahamu na kujua kiwango cha ladha hii.
0 Comments