NAMNA YA KULEA VIFARANGA

KARIBU TENA KWA AWAMU NYINGINE KATIKA MASUALA HAYA YA UFUGAJI
Waondoe vifaranga kwenye nyumba au kitalu cha kuwalea mara tu wakiwa na
manyoya ya kutosha, yaani katika juma la 4 -5 kutegemeana na hali
yao ya manyoya na hali ya hewa iliyopo.
Ulishaji wa Vifaranga
Chakula na Maji
Ili vifaranga wawe na maendeleo mazuri ya ukuaji, wanatakiwa wapewe chakula chenye
virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini ambavyo ni Protini, Madini, Wanga na Vitamin
pamoja na maji safi wakati wote.
• Pia chakula kunaweza kuchanganywa na mchanga kidogo ambao husaidia usagishaji
wa chakula kilicholiwa.
• Hakikisha vyombo vya maji vinakuwa safi wakati wote.
• Chakula na maji yabadilishwe kila baada ya masaa 24.
• Hakikisha vifaranga wanapewa chakula wanachoweza kumaliza katika masaa 24 ili
kuzuia uharibifu.
Siku 7 – 10 baada ya kupokea vifaranga vyombo vya mwanzo vya maji na chakula
vibadilishwe wawekewevyombo vya kawaida.
Vifaranga wapewe maji safi , vyombo vya maji visafi shwe na kujazwa maji mara mbili kila
siku. Kila asubuhi sehemu zilizo na vyombo vya maji zikaguliwe na takataka zenye unyevu
ziondolewe.
Vyombo vya chakula vijazwe nusu hasa vifaranga wakiwa na umri wa siku 10 – 14. Pia
vifaranga wakiwa na umri huo huo wapewe majani mabichi yaliyo bora na yenye thamani.
Majani yafungwe mafungu na kuning’inizwa kwa kamba.
Vyombo vya chakula na maji
Vyombo vya chakula na maji vinaweza kuwa
ni makopo, sufuria, karai n.k. Pia vinaweza
kuundwa kwa kukata madebe, galoni za
plastiki, vibuyu n.k.
Aidha vyombo hivyo
vinaweza kutengenezwa kwa kutumia mbao,
mianzi, Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa
vyombo hivyo haviruhusu kuku kuchafua
chakula au maji.
Mfano wa vyombo vya
chakula na maji ambavyo mfugaji anaweza
kujitengenezea.
FUATILIA:: HHANDOS BLOG.COM KWA UJUZI ZAIDI,,,

Post a Comment

0 Comments