MAGONJWA YA KUKU NA NAMNA YA KUYATIBU / KUYAKINGA


Hakuna ufafanuzi unaopatikana wa picha.

karibu tena kwa utambunzi wa magonjwa yanayo sumbua sana  kukuna matibabu yakee  
Ugonjwa unaosumbua sana wafugaji wa kuku ni Mdondo na wengine huuita Kideri (new
castle disease). Chanzo cha ugonjwa huu ni virusi.
Ni ugonjwa unaoathiri kuku wa rika zote
na mara nyingi humaliza kuku wengi au wote vijijini.
Dalili za Mdondo ni:
• Kuku hukohoa
• Kuhema kwa shida
• Hushusha mbawa
• Kupoteza hamu ya kula, kuzubaa, kusinzia
• Manyoya kuvurugika
• Kuharisha kijani
• Kutokwa ute mdomoni na puani
• Kizunguzungu, shingo kujikunja, kurudi kinyumenyume, kupooza mabawa, kuanguka
chali, kupoteza fahamu na hatimaye kufa.
• Kuku wengi kwenye kundi hufa katika kipindi kifupi kwa kufikia asilimia 90 hadi 100.
Uenezaji wa ugonjwa huu ni kwa njia zifuatazo:
• Kinyesi cha kuku anayeumwa kikikanyagwa na miguu, magari, baiskeli na kuwafikia
kuku nwengine.
• Kwa njia ya hewa (kuvuta hewa yenye virusi ) au upepo waweza kusafirisha virusi.
• Mabaki ya kuku anayeumwa kama utumbo, manyoya n.k. visipozikwa vitaeneza
ugonjwa kwa kuku wazima kula mabaki hayo au wanyama watakaokula mabaki hayo
huweza kuyasambaza na kueneza ugonjwa.
Kudhibiti Mdondo
Kuchanja
Kwanza kabisa ni chanjo ya Mdondo.
Zipo aina tofauti za chanjo ya Mdondo. Lakini chanjo iliyo rahisi kutumiwa vijijini inaitwa I-2
Thermostable. Chanjo hii tofauti na chanjo nyingine nyingi inao uwezo wa kustahimili joto.
Hutolewa kwa njia ya kuku kudondoshewa tone moja la dawa katika jicho moja tu. Hii ni dozi
kamili kwa kuku wa umri wowote.
Pia chanjo maarufu kwa mijini ni Newcastle ambapo huchanganya na maji kisha unaweka kwenye vinywesheo kwa muda wa massa mawili


madunga vetagro limited ni suluhisho lako la hayo yote apo juu,,kwa mawasiliano zaidi tucheki  kwa hii number,,0782707740,0625605384

Post a Comment

0 Comments