Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Kigwangala amesema Serikali itaanza kuuza asilimia 10 ya mamba nje ya nchi kwa kile alichokieleza kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wanyama wakali kuingia kwenye makazi ya watu.
Waziri amesema Serikali imejhitahidi vya kutosha kuhakikisha suala la ujangiri linaisha na nchini na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa bali changamoto iliyopo, ni wanyama hao kuingia kwenye makazi ya watu.
“Uhifadhi na ulinzi wa maliasili nchini umeimarika na tumepata mafanikio makubwa sana. Ujangili tumeudhibiti kwa mafanikio makubwa sana“ Waziri Kigwangalla
“Changamoto mpya imezaliwa, wanyama wakali na waharibifu wamezidi na wanavamia maeneo ya watu, tumeamua kuuza asilimia 10 ya mamba wote nchini!” Waziri Kigwangalla
Aidha Waziri Kigwangala amesema pia Serikali itauza viboko wote waliopo kwenye maeneo yenye maji kama maziwa, mabwawa na mito iliyopo mjini.
0 Comments