Serikali imewachagua wanafunzi 1,674 kujiunga kidato cha tano baada ya awamu ya kwanza kukosa fursa hiyo.
Awali, serikali ilitangaza kuwa wasichana wote waliofaulu kidato cha nne walichaguliwa kujiunga vyuo mbalimbali pamoja na kidato cha sita lakini wavulana 1,861 hawakuchaguliwa licha ya kuwa na sifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametangaza hayo leo, Jumatano (Agosti 28, 2019), jijini Dodoma huku akisema kuwa 187 wamekosa kwa kukosa uwiano katika tahasusi zao.
Waziri Jafo amesema wanafunzi hao wanatakiwa kuanza kuripoti katika shule walizochaguliwa kuanzia Septemba 2 hadi 16,2019 huku akiwataka waliokosa nafasi kutokata tamaa badala yake waombe vyuo vya kati ili wajiunge.
Ametaja sababu za kupatikana kwa nafasi ni kutokana na baadhi ya wanafunzi kujiunga shule binafsi na baadhi ya shule zimeongeza majengo
0 Comments