Upungufu wa damu mwilini (Anemia)

Anemia au Anaemia ni hali inayotokea pale kiasi cha seli nyekundu za damu zinapokuwa chache kuliko kawaida au seli hizi nyekundu zinapungukiwa na chembechembe za hemoglobin. kwa lugha rahisi tunasema ni upungufu wa damu mwilini. Kuishiwa damu hupelekea mwili kuwa mchovu muda mwingi, misuli kuishiwa nguvu, mood kubadilika na kupata ganzi mara kwa mara. Tatizo linavokuwa kubwa zaidi linaweza kupelekea matatizo kwenye moyo, ubongo na viungo vingine vya mwili

Anemia ni nini?

Anemia ni hali ya upungufu wa chembechembe ya hemoglobin kwenye seli nyekundu za damu. Hemoglobin ni aina ya protini iliyoundwa na madini ya chuma kwa wingi inayohusika na kusafirisha hewa safi ya oxygen kwenye damu.  Chembechembe hii ndio inayoipa damu wekundu wake. Kumbe basi kwa maelezo haya ni kwamba mtu mwenye Upungufu wa damu (anemia) anapata upungufu wa hewa ya oxgen mwilini kutokana na kwamba vibeba oxygen ni vichache. Pia chembechembe hizi za hemoglobin zinahusika katika kupambana na maradhi, kuganda kwa damu na hizo kuzuia damu kuvuja sana pale mtu anapopata ajali.
Upungufu wa madini ya chuma ni chanzo kimojawapo cha kupungukiwa damu mwili kwa mujibu wa taasisi ya kupambana na magonjwa ya Marekani (Center of disease control). Wanawake ni kundi lenye hatari zaidi kupata upungufu huu wa damu kutokana na hedhi. hivo kuna umuhimu wa kuruisha madini ya chuma yanayopotea kwa kula zaidi vyakula vyenye madini ya chuma.

Dalili kuu za Upungufu wa Damu Mwilini

Pasipo uwepo wa vibeba oksijeni kwenye damu, maeneo mbalimbali ya mwili yatakosa hewa na kupeleka ufanisi kupungua, sehemu hizi ni misuli, viungo kama moyo na ubongo, tishu mbalimbali na seli za mwili. Dalili kuu ni kuhisi umechoka na mwili kutokuwa sawa muda mwingi. Zifuatazo ni dalili za upungufu wa damu (anemia)
  • Mwili kukosa nguvu na uchovu wa mara kwa mara
  • Mapigo ya moyo kubadilika badilika na moyo kwenda mbio sana
  • Kupumua kwa shida na stamina kupungua
  • Maumivu ya kifua
  • Kusinzia sana na mwili kutokuwa sawa
  • Mikono kuwa ya baridi na
  • Kupata maumivu ya kichwa
Muhimu kufahamu ni kwamba anemia huanza taratibu bila kuonesha dalili zozote lakini tatizo huwa linazidi kuwa kubwa kadiri muda unavoenda na hasa pale ikiwa kuna vitu hatarishi zaidi ya kimoja vinavyopelekea anemia.
Kuna sababu kuu tatu za kwanini umepata anemia (upungufu wa seli nyekundu za damu) ambazo ni mwili kutotengeneza seli nyekundu za kutosha, kupoteza damu nyingi kwenye ajali na mwili wenyewe kupambana na seli nyekundu za damu. Hapa chini ni mazingira na vihatarishi vinavyopelekea anemia
  • Upungufu wa madini ya chuma au Vitamin B12. Hii inaweza kukutokea endapo unaaacha kula baadhi ya chakula, au kwa watu wasiokula kabisa nyama na mazao ya wanyama.  Mwili unahitaji zaidi madini ya chuma na Vitamin B12 ili kutengeneza chembechembe za hemoglobin.
  • Wanawake wapo kwenye hatari zaidi ya kupata upungufu wa damu kuliko wanaume kutokanana kupoteza damu nyingi kipindi cha hedhi.
  • Wazee na wenye umri mkubwa. Tafiti zinasema kwamba watu wenye umri zaidi ya miaka 65 wapo kweye hatari zaidi ya kupata upungufu wa damu.
  • Wajawazito
  • Ukuaji wa fangasi wa candida kupita kiasi hupunguza uwepo wa mwili kufyonza Vitamins.
  • Magonjwa ya autoimmune ambapo kinga ya mwili inashambulia seli za mwili, saratani, Ukimwi, Figo
  • Matatizo kwenye mfumo wa chakula yanayopelekea uchakataji wa chakula kuvurugika na mwili kushindwa kuvyonza madini na vitamin za kutosha.
  • Kumeza vidonge mara kwa mara mfano vidonge vya kupunguza maumivu hasa asprin.

Mchango wa Lishe Mbaya Kwenye Upungufu wa Damu.

Kuna kitu cha msingi zaidi unatakiwa kufanya kwenye lishe yako, ukiachilia mbali kula vyakula vyenye madini ya chuma ni muhimu pia kuacha kutumia vyakula vilivyosindikwa kiwandani kama nafaka iliyosafishwa, sukari na vyakula vya makopo, vyakula hivi kuleketeza mcharuko (inflammation) kwenye mwili, uzito mkubwa na kitambi, mwili kuwa mchovu na mwili kushambuliwa mara kwa mara na bacteria na fangasi.
Fangasi wa Candida wanapokuwa kupitia kiasi huvuruga pH na utando laini kwenye tumbo na utumbo na hivo kupekelea sumu na vitu visivyohitajika kuingia kwenye damu kupitia ukuta wa tumbo. Magonjwa mbalimbali ya mfumo wa chakula kama leak gut, Irritable bowel syndrome na pia anemia huletekezwa na kuvurugika kwa mazingira ya tumbo. Kama unapata dalili za weupe kwenye ulimi au kwenye koo basi hizi ni kiashiria kwamba una fangasi.

List ya Vyakula Unavyotakiwa Kuepuka Kama una Upungufu wa Damu

  • Sukari iliyoongezwa kwenye vyakula na vinywaji
  • Nafaka zilizokobolewa
  • Maziwa yaliyosindikwa kiwandani
  • Soda: soda ina sukari nyingi, haina virutubisho vyovyote na huzuia ufyonzaji wa madini ya chuma mwilini.
  • Kahawa na chai nyeusi: unywaji wa kahawa kupita kiasi huzuia ufyonzaji wa madini ya chuma mwilini.

Hatua Tano za Kuongeza Damu Mwilini

  1. Hatua ya kwanza ni Kuimarisha ufanyaji kazi wa Bandama :Bandama ni kiungo kinachohusika na utengenezwaji wa seli nyekundu  za damu na pia kuweka msawazo wa majimaji mwilini. kama bandama yako ina shida basi hii ni sababu ya kwanza kwanini una upungufu wa damu mwilini.
    Tumia vyakula vifuatavyo ili kuweka sawa bandama yako.vyakula kama spinach na mboga zingine za kijani, maboga na mbegu za maboga na karanga.
  2. Hatua ya pili ni kuimarisha mfumo wa chakula: Hatua ya kusafisha na kuimarisha mfumo wa chakula ni muhimu sana kutokana na kwamba unaweza kula vyakula vyenye madini chuma kwa wingi lakini mwili ukafeli kuvyonza madini kuingia kwenye damu. Tatizo ni kwamba una hali inayoitwa leaky gut syndrome.
    Angalia mfano huu ili unielewe kuhusu leky gut syndrome. Utumbo mwembamba ndio huusika na uchakataji wa chakula na kisha virutubisho muhimu kuruusiwa kuingia kwenye damu na makapi zikiwemo sumu, virusi, bacteria na vimelea wabaya kutolewa nje. Sasa ukuta huu ni kama chekecheke linachuja vitu vizuri na vibaya.
    Chekecheke hili linapotoboka kutokana na ulaji wa vyakula hatarish na uwepo wa fangasi linaanza kuruhusu sumu na vitu hatari kuingia kwenye damu, kitendo hichi cha kutonoka kwa chekecheke kwenye utumbo na tumbo tunaita leaky gut na mkusanyiko wa dalili mbaya zinazotokana na sumu, vimelea na takataka kuingia kwenye damu kama alegi, kichefuchefu na mwili kutosaga chakula vizuri tunaita leaky gut syndrome.
    Hii ni hatua ya pili katika kukarabati mfumo wako wa chakula ulioharibika kutokana na lishe mbaya. Unaweza kujaribu digestive package care yetu itakusaidia, kusafisha tumbo, kuongeza bacteria wazuri tumboni na hivo kuimarisha usagaji na ufyonzaji wa virutubisho.
  3. Hatua ya tatu ni kutumia kwa wingi vyakula vyenye madini ya chuma: Hatua inayofuata katika kuimarisha utengenezwaji wa seli nyekundu za damu ni kuongeza kweye sahani yako vyakula vyenye madini chuma kwa wingi. Vyakula hivi ni kama Nyama, samaki, karanga, maharage na mboga za kijani kama spinach. viungo kama maini ya madini chuma kwa wingi zaidi.
  4. Hatua ya nne ni Kupunguza msongo wa mawazo: Kama unapata msongo wa mawazo, hasira, hofu na kushindwa kusamehe watu basi  unapunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa bandama yako. Hivo hakikisha unakuwa na ratiba ya kupumzika na kufurahia maisha, na kupata usingizi wa kutosha. Unaweza kufatilia njia salama za kukabiliana na msongo wa mawazo hapa.
  5. Hatua ya tano: Kutumia virutubisho ili kuongeza uzalishaji wa damu mwilini . Virutubisho hivi ni kama Vitamin B complex. Tumia pia mimea tiba ya wachina (chinese traditional medicine) kama Ginseng na Spiriluna na marrow powder zenye madini ya magnesium na chuma kwa wingi. 
green world spiriluna
Spirulina
Compound marrow
marrow powder
Green world Ginseng
Ginseng

Maelezo ya Mwisho Kuhusu Anemia

Japo unaweza kutubu tatizo la kuishiwa damu ukiwa nyumbani kwa kurekebisha lishe kuna umuhimu pia wa kuongea na dactari wako akupe mwongozo na ushauri wakati unaendelea na lishe. Ni muhimu kupata usaidizi wa Dactari kutokana na kwamba kuishiwa damu inaweza kuwa ni dalili ya tatizo kubwa la kiafya