Leo nimeamua kuomba ushauri katika hili, maana sasa naona si kawaida

Nilikua na maisha ya kawaida na yenye uhakika nikiwa mwajiriwa na pia kua shughuli ndogo nikiziendesha hapo hapo kazini zilizokua zinanipa kipato. Nilikua na rafiki wa kike ambae tulikujaingia katika mahusiano na kupelekea kupata ujauzito na kwakua ni kosa tushafanya nililazimika kuilea mimba mpaka kuzaliwa mtoto jambo ambalo lilinipitisha katika wakati mgumu kutoka na maradhi kwa mwenzangu nilijituma kiasi nikauza baadhi ya vitu ili aweze tibiwa, akapona tukaanza maisha tuko wakati huo tulipisha kauli mara kwa mara nikawa mvumilivu

Baada ya uzazi nilimtaka afanye kazi nae asikae tu nyumbani lakini hakutaka akawa na sababu mtoto.wakati huo mtoto ana miaka miwili na mtoto alimpenda bibi ake (mama yangu ) sana hadi kupendelea kushinda kwake. Mke nilimwambia nafasi hiyo aitumie basi kufanya kazi alichagua atafungua genge mimi nikaona kuliko genge akaombe baraza za watu bora nimkodie frame atayoweka genge na pia kuwe na duka hapo ajipatie kipato

Kuna wakati mimi kama mume nilipenda kujua maendeleo ya biashara hiyo na alipokwama lakini hakutaka kabisa ila aliomba fedha nimwongeze alipo kwama. baada ya muda niliamua nitaenda cheki amefikia wapi kuna kuendelea au la kwa bahat mbaya nilikuta dukan lilikua likifa polepole nilipomuuliza wapi pesa unapeleka usiendeleze biashara hii. Alinijibu nisimfuatilie ka nimemfungulia biashara kwa jibu lile nilikaa kimya siku zilipita sikutoa tena pesa kumwongezea dukan baadae aliniambia tu lileduka kafunga na kauza vitu vyote

Nilianzishia biashara nyingine ambayo ilitoa faida 100% nilijaribu mshawish aifanye hakutaka akawa ye ni misele na vikundi vikoba baada ya muda alipokosa marejesho akaomba anisaidie nikamwachia biashara hiyo ambayo nilimwambia mtaji inayo wetu ukijituma utalipa marejesho yako na utabakiwa na pesa nyingi mi nikaenda tafuta shughuli ingine baada ya muda ile biashara ikafa kutokana na yeye kutohangaika nayo na wateja wote wakahamia kwingine.

Kwasasa yeye safari ni nyingi kwenda kwao, akirudi tu wmwenye kiburi anakuwa na tabia za udokozi nk huku akisema yeye alichofata ni pesa tu na si kingine nikiongea na wazazi wake wamshauri nao wanakuwa kama wanamtetea na kusema mtoto wao anaweza kuolewa na mtu yoyote yule

Mpaka sasa sina maelewano na huko kwao baada ya kuacha watumia fedha za matumiz wakanichukia hata kunitukana sasa hivi kazini nilisimamisha sababu niliyoambiwa na rafiki yangu mabosi wanadai mke nilie nae ananirudisha nyuma na hanaa msaada kwangu.

Marafiki nao wananikimbia na kunitenga sababu tu ya mke nilie nae naombeni ushauri wenu mimi ni kijana mdogo huenda ninyi mshakutana na haki kama hizi au kusikia popote pale