Viongozi wanane wa Chama cha ACT-Wazalendo, mkoani Lindi wanawashikilia kwa mahojiano na Jeshi la Polisi  kwa madai ya kufanya mkusanyiko usio halali wa kutokuwa na kibali kutoka kwa jeshi hilo

Wanaoshikiliwa ni Mwenyekiti wa Chama hicho, Rashidi Mchinjita, Hamisi Sapanga {Katibu Mipango na uchaguzi}, Deo Chaurembo (Katibu Mwenezi Mkoa),Pili Salum Nguru (Mjumbe), Rukia Abdallah (Mwenyekiti Ngome ya Wanawake) na Zuhura Hemedi (Katibu Wanawake Ngome).

Viongozi wengine ni Rajabu Nakanganigwe (Katibu Itikadi Jimbo), Katibu Mipango na uchaguzi Jumbo) na Shuwea Ahamadi Chinangalile (Katibu ngome ya vijana Mkoa).

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Lindi, ACP Prodansiana Protas akizungumzia kuhusiana na tukio hilo, amesema Jeshi la Polisi linawashikiria kwa sababu watu hao walikuwa wakifanya maandamano, kinyume na sheria za nchi.

Hata hivyo, Katibu wa Wazee wa ACT-Wazalendo, Jimbo la Lindi Mjini, Mussa Pinda Chikupi, amesema baada ya uzinduzi wa Kizimba, waliingia ndani kuendelea na kikao chao, wakati wakiendelea askari 5 wa Jeshi la Polisi wakiwa wamevalia nguo za kiraia, walifika eneo hilo wakiwa na gari ndogo aina ya Toyota Cruser na nkuwaamuru kwenda kituoni.