Inaripotiwa kuwa Mabingwa wa ligi kuu nchini Ubelgiji, KRC Genk wamemsajili mshambuliaji wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya FC Midtjylland, Paul Onuachu kwa dau la pauni milioni sita (6).
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, ni mbadala wa mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta ambaye anadaiwa kukaribia kuondoka katika klabu hiyo msimu huu.
Kijana huyo wa The Super Eagles amefanikiwa kufanya vizuri mno kwenye michuano ya Africa Cup of Nations iliyomalizika hivi karibuni nchini Misri ambapo alifanikiwa kuondoka na Medali ya shaba baada ya kuisadia timu yake ya taifa kushinda mshindi wa tatu kwa kuifunga Tunisia kwa bao 1 – 0.
See Sports Radio 88.9 Brila FM's other Tweets Inadaiwa mchezaji huyo kuwa sehemu ya usajili mkubwa miongoni mwa wachezaji wa Nigeria waliyosajiliwa msimu huku thamani yake ikitrajiwa kuongezeka.
Paul Onuachu alijiunga na FC Midtjylland wakijulikana kwa jina la utani Wolves mnamo mwaka 2012 na kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 70 katika michezo 181 aliyoshiriki kwa michuano yote. Akifunga mabao 22 na kupiga pasi za mwisho zilizochangia magoli (assists) 40 kwenye mechi zake za mwisho wa msimu.
0 Comments