BAADA ya hivi karibuni mabeki wa kati wa Simba, Pascal Wawa na Erasto Nyoni kufanya makosa kadhaa katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, wachezaji hao jana waliwekwa kitimoto na kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems.
Aussems amefi kia hatua hiyo ili kuhakikisha wachezaji hao wanajirekebisha kabla ya kupambana na UD Songo ya Msumbiji katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afi rka.
Mchezo huo umepangwa kuchezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na timu zote zitashuka uwanjani zikiwa na kumbukumbu ya kutofungana katika mchezo wa kwanza uliochezwa huko nchini Msumbiji.
Erasto Nyoni
Habari za kuaminika kutoka katika timu hiyo ambazo Championi Jumatano limezipata, zimedai kuwa Aussems alikutana na wachezaji hao baada ya mchezo wao huo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.
“Kuna makosa ambayo walikuwa wakiyafanya katika mchezo ule ambayo kama Azam wangekuwa makini hakika wangefunga mabao mengi.
“Kwa hiyo kutokana na hali hiyo kocha alikutana nao na kuzungumza nao juu ya mapungufu hayo na kuwataka kubadilika na kuongeza umakini zaidi katika mechi yetu ijayo dhidi ya UD Songo,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Aussems alisema kuwa: “Ni kweli baada ya mechi hiyo nilikutana na wachezaji wote na kuwaambia mapungufu ambayo yalijitokeza katika mchezo huo na nikawakumbusha kuwa makini zaidi. “Hata hivyo, tunaendelea na maandlizi yetu kwa ajili ya mechi yetu ijayo na ni matumaini yetu kuwa kila kitu kitakuwa sawa.”
0 Comments