MTOTO JAMBAZI SUGU AKAMATWA HUKOO CONGO



Kijana Pasi Daniel Simuzizi mwenye umri wa miaka 14 amekamatwa na idara za ujasusi za jeshi la FARDC baada ya mwenzake kutoa habari kwa vyombo husika jijini luberizi tarafani uvira mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya CONGO,

Duru za habari zaendelea kusema kwamba ; kijana Pasi alikuja kumchukua rafiki yake ambaye alikwa amebaki kijijini ili naye amfuate waishi pamoja msituni ndipo kijana huyo akavujisha siri na kwenda kwenye kituo cha jeshi na kuja kumkamta,

Duru mbalimbali zaeleza kuwa mtoto huyo alizaliwa msituni katika maisha ya kushika silaha,kazi hiyo ya kupiga silaha aina ya kalashenikov maarufu AK47 ameirithi kwa baba yake ambaye amekwisha fariki,

wengi walimfahamu kwa jina la simuzizi alikuwa akiongoza kundi la wapiganaji la maimai simuzizi, kundi hilo lilikuwa hatari wakati wa miaka 2010,kwenye bonde la mto ruzizi,

Kijana Pasi Daniel Simuzizi alikuwa akitumika na kundi la wanamgambo FNL kutoka Burundi likiongozwa na Nzabampema ambaye awali alihudumu kwenye jeshi la taifa la Burundi (FDN) na kabla ya hapo meja alois Nzabampema alikuwa kamanda wa kanda ya kwanza ya kijeshi kwenye kundi la FNL palipehutu chini ya uongizi wa Agathon Rwasa.

Kundi hilo la FNL limekuwa likiendesha uporaji na mauaji dhidi ya raia wa kandokando na mpaka DRC na Burundi.

Duru za habari zinaendelea kusema kwamba ; pasi Daniel Simuzizi amekuwa mara kwa mara akiendesha vitendo hivyo vya uporaji na utekaji nyara hasa watu wenye muonekano wa kipesa na kuwaacha baada ya familia zao kutoa kiwango cha pesa ambacho walichokiomba,ili kufadhili kundi hilo la FNL la meja aloise nzabampema.

Eneo hilo la bonde la mto ruzizi na milima inayoinukia bonde hilo,maeneo hayo yamekuwa ni uwandja wa mapambano kati ya makundi ya maimai kwa ushirikiano na makundi ya redtabara na FNL kutoka Burundi, kwa upande mwengine jeshi la Burundi kwa ushirikiano na vijana imbonerakure wanaoegemea chama tawala CNDD\FDD limekuwa likinyooshewa kidole na mashirika ya kutetea haki za binadam kwa kuingia bonden huko kwenye ardhi ya kongo kuwasaka waasi hao.

Post a Comment

0 Comments