MAREKANI WAENDELEA NA KUTESTI MAKOMBORAA YAO ANGALIA


Marekani imefanyia jaribio kombora lake la masafa ya kadri wiki kadhaa baada ya kujiondoa katika makubaliano muhimu na Urusi yaliopiga marufuku silaha zenye uwezo kama huo za kinyuklia.

Pentagon imesema kwamba ilifanikiwa kurusha kombora hilo katika pwani ya California siku ya Jumapili.

Marekani ilijiondoa katika makubaliano hayo mnamo tarehe 2 Agosti baada ya kuishutumu Urusi kwa kulikiuka azimio hilo madai ambayo Moscow imekana.


Wachanganuzi wanohofia kwamba kuanguka kwa makubaliano hayo kutazua ushindani wa utengenezaji wa silaha mpya.

Makubaliano hayo yalioafikiwa katika kipindi cha vita baridi yalipiga marufuku silaha zenye uwezo wa kurushwa kati ya kilomita 500 hadi 5,500.

Pentagon imesema kwamba kombora hilo lililofyatuliwa kutoka kisiwa kinachodhibitiwa na wanamaji wa Marekani cha San Nicolas katika pwani ya Los Angeles, lilikuwa halina kichwa cha kinyuklia.

Silaha hiyo iliofanyiwa majaribio iliafikia lengo lake la zaidi ya kilomita 500, kulingana na idara ya ulinzi nchini Marekani.

Data iliokusanywa na mafunzo kutoka katika jaribio hilo itaelezea idara ya ulinzi kuhusu uundaji wa silaha za masafa ya kadri katika siku za usoni kuhusu uwezo wake.

Je ni nini kitakachofanyika na makubaliano hayo?
Urusi imeshutumiwa kwa kukiuka masharti ya mkataba huo katika siku za nyuma, lakini mapema mwaka huu, Marekani na Nato ilisema kwamba kulikuwa na ushahidi kwamba Moscow ilikuwa na mpango wa kurusha kombora jipya aina ya 9M729 linalojulilkana na Nato kama SSC-8.

Urusi imekana shutuma hizo na rais Putin alisema kwamba Marekani ilifanya makosa makubwa kujiondoa katika makubaliano hayo.

Mnamo mwezi Februari rais Trump aliweka siku ya mwisho ya Agosti 2 kwa Marekani kujiondoa katika makubaliano hayo iwapo Urusi itaendelea kukiuka masharti yake.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alipiga marufuku makubaliano ya taifa lake katika mkataba huo muda mfupi baadaye.

Marekani ilijiondoa katika makubaliano hayo baada ya kutishia kufanya hivyo mnamo tarehe 2 Agosti na waziri wa maswala ya kigeni Mike Pompeo alisema: Urusi ndio ya kulaumiwa kwa kuanguka kwa mkataba huo.

Post a Comment

0 Comments