Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali mapingamizi ya Serikali kupinga kusikilizwa kwa maombi ya kesi namba 18/2019 ya Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kuhusu ubunge wake kwa sababu hazina mashiko.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Agosti 26,2019 na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Jaji Sirillius Matupa wakati akitoa uamuzi wa pingamizi la awali dhidi ya maombi ya Lissu lililowekwa na Serikali katika maombi yake ya kibali cha kufungua shauri ili kupigania ubunge wake.
Kutokana na hatua hiyo, maombi ya Lissu kutetea ubunge wake wa Singida Mashariki yataendelea kusikilizwa mahakamani hapo mbele ya Jaji Sirilius Matupa.
0 Comments