KUJENGA MWILI NI JUKUMU LAKO,, BAC MABOGA NI KIBOKO YAO FOLLOW ME






MABOGA hutokana na tunda liitwalo boga. Tunda hilo asili yake haijafahamika vizuri ingawaje baadhi ya tafiti zinasema asili yake ni Amerika Kaskazini.
Maboga ni moja ya chakula bora na muhimu kwa siha ya mwili wa mwanadamu endapo yataandaliwa vizuri.
Leo tutajali zaidi faida ya mbegu za maboga ambazo zina kiwango kingi cha protini na vitamini.
Mbegu hizo zinaweza kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu na kwamba gramu moja ya mbegu za maboga huwa na protini sawa na glasi moja ya maziwa.
Watu wengi wanaweza kudharau mbegu za maboga pengine kwa kutokufahamu faida zake, lakini ukweli ni kwamba ni miongoni mwa mbegu zenye faida kubwa mwilini, kwani huweza kuzuia na kutibu hata baadhi ya magonjwa hatari yaliyoshindikana hospitalini.

Zina madini aina ya zinc, kopa, magnesium, chuma , manganese, phosphorus
Husaidia uzalishaji wa Maziwa kwa mama anaenyonyesha
Husaidia kurekebisha sukari mwilini na kuwezesha kongosho kufanya kazi yake vizuri
Huimarisha mfumo wa uzazi kwa wanaume na wanawake kutokana na madini aina ya zinc omega3 na omega6
Huondoa sumu mbalimbali mwilini hasa kwenye figo na kibofu cha mkojo pia huondoa madhara ya pombe kiafya

Ni chakula bora kwa mama mjamzito
Husaidia kuondoa shinikizo la damu

Ni chanzo kizuri cha vitamin K, A ,B,E
Ni kinga dhidi ya kansa ya kizazi kwa wanaume na wanawake
Huboresha kumbukumbu, akili kwa watoto na watu wazima

Husaidia kutibu matatizo ya viungo
Husaidia kuondoa unene unaotokana na wingi Wa mafuta cholesterol mwilini

Ni kinga tiba dhidi ya moyo INI na figo

Husaidia kutibu matatizo ya macho kutokana na wingi Wa vitamin A

Huimarisha mishipa ya sehem za siri kwa wanaume na kufanya iwe na nguvu Mara dufu kutokana na madini aina ya zinc,, chuma na kopa 

Kula mbegu za Maboga kwa faida kubwa mwilini


Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha zinc, tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya mbegu zenyewe za maboga huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya kibofu.
Mbali na hayo, mbegu hizo zina virutubisho vinavyotoa kinga dhidi ya magonjwa ya ini na moyo.

Hali kadhalika mbegu za maboga zina virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa yote ya uvimbe mwilini, ikiwa ni pamoja na kuvimba miguu, vidole na hata majipu.

Mbegu za maboga pia ni chanzo kizuri cha kamba lishe, kutokana na sifa hiyo boga linaweza kuwekwa kwenye orodha ya vyakula ambavyo husaidia kuondoa tatizo la ukosefu wa choo au kupata choo kigumu.

Mbegu za maboga zina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Mbegu za maboga zimethibitika kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vya aina mbalimbali kama vile magnesium, manganese, shaba, protini, zinki nakadhalika.

 Zifuatazo ni baadhi ya faida za matumizi ya mbegu za maboga.
Pamoja na faida zilizo tajwa hapo jua ,nyinginezoo ni kama ifuatavyo,,,
  1. Kuongeza maziwa kwa wanawake wanaonyonyesha Kwa wanawake wanaonyonyesha matumizi ya mbegu za maboga huwasaidia kuongeza kiwango cha maziwa yenye afya kwa watoto wanaonyonya
  2. .Mbegu za maboga zina kiwango kikubwa cha vitamini c.Pia zina madini ya magnesium ambayo mwanadamu anatakiwa kuyatumia kila siku.
  3. Licha ya boga lenyewe kuliwa, mbegu za maboga zina kiwango kikubwa cha madini ya zinc ambayo yana faida mbalimbali katika mwili wa mwanadamu kama vile 
  • kuimarisha kinga ya mwili, 
  • kuimarisha uwezo wa kuonja na kunusa, 
  • ukuaji wa seli mbalimbali za mwilini, 
  • kuimarisha afya ya macho na ngozi, 
  • kulinda na kuimarisha insulin pamoja na
  •  kuongeza uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa wanaume.

Mbegu za maboga ni miongoni mwa vyanzo bora kabisa vya mafuta na acid zitokanazo na mimea ambazo zina faida kubwa sana kwa afya ya mwili wa mwanadamu.
Pia zinasaidia katika kulinda na kuimarisha ufanisi wa tezi kwa wanaume,

Mbegu hizo zina faida kubwa sana kwa wagonjwa wa kisukari kwani zinasaidia katika kulinda, kuboresha, kuimarisha na kurutubisha insulin.
Mbegu za maboga zina imarisha na kulinda afya ya moyo na ini.

Pia zinasaidia katika kuboresha usingizi. Kama una matatizo ya usingizi unashauriwa kutafuna mbegu za maboga pamoja na tunda kidogo. Hii itakusaidia katika kupata usingizi mzuri.
Anza kujenga tabia ya kuwa unatumia mbegu za maboga kwa faida mbalimbali kwa afya ya mwili wako kama ilivyoonyeshwa hapo juu.

Matumizi ya boga pia husaidia kuongeza unyevunyevu kwenye ngozi na hivyo kuwasaidia wale wenye matatizo ya ngozi kavu hii ni kutokana na boga kuwa na vitamin E ya kutosha pamoja na kirutubisho kiitwacho ‘antioxidant’.
Maboga yenyewe pia yana vitamin ‘A’ ya kutosha ambayo husaidia kulinda ngozi dhidi ya kuharibika na kuunda seli mpya ndani ya ngozi. Pia ndani ya boga kuna vitamin C ambayo nayo huhitajika sana katika kuhakikisha afya ya ngozi inakaa vizuri zaidi siku zote.

FUATILIA NAKALA HII KUOKOA AFYA YAKOO
Asanteni
maboga-1-1024x682-jpg.762619

Post a Comment

0 Comments