faida za tangawizi kwa afya zetu




Karibu tena msomaji wangu leo ningependa kukushirikisha faida zinazopatikana katika tangawizi japo wengi wetu tunaifahamu kama dawa ila atufahamu faida zake zote leo ningependa uzifahamu faida za tangawizi.
Karibu twende pamoja.
Faida mbalimbali za tangawizi ni:

  1. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini ambazo zimo ndani ya mwili na juu ya ngozi.
  2. Kuna  (antibiotics) ya asili kwenye tangawizi, hivyo huondoa sumu mwilini haraka.
  3. Tangawizi ina uwezo mkubwa sana wa kuondoa uvimbe mwilini.
  4. Ndani ya  Tangawizi kuna zingibain ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake
  5.  Huondoa maumivu mbalimbali mwilini na pia, Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)
  6. Tangawizi ina uwezo wa kutibu saratani ya tezi dumeTangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seliza kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa (4) manne kimeng’enya hicho kikikosekana.
  7.  Tangawizi  huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol
  8. Tangawizi ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia) pia ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)
  9.  Tangawizi huzuia kuzalish kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidondavya tumbo mwilinipia hutibu kiunguliana kanza mbalimbali za tumbo
  10. Tangawizi ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi, Hutibu kanza za kwenye kizazi na kanza zakwenye mirija ya uzazi.
  11. Tangawizi huongeza msukumo wa damu, Husaidia kuzuia shambulio la moyo
  12. Huzuia damu kuganda.
  13.  Hushusha kolesto
  14. Husafisha damu.
  15.  Hutibu shinikizo la juu la damu
  16.  Husafisha utumbo mpana
  17. Huondoa gesi tumboni na pia husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vizuri.
  18. Kwa wale wenye uchovu basi tumia kikombe kimoja cha tangawizi nawe utakuwa imara tena
  19. Tangawizi husaidia kuzuia kuharisha
  20. Husaidia mfumo wa upumuaji na kupunguza tatizo la  pumu
  21.  Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto, Hutibu homa ya kichwa.
  22. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi
  23. Tangawizi Huimarisha afya ya figo.
  24. Tangawizi ina madini ya potassium ya kutosha pia ina madini ya manganese ambayo ni muhimu katikakuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.
  25.  hulinda kuta za moyo.
  26. hulinda mishipa ya damu na mishipa ambayo mkojo hupita.
  27. Tangawizi ina ‘silicon’ ambayo kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozinywelemeno na kucha.
  28. Tangawizi ina uwezo mkubwa sana wa kuongeza nguvu za kiume.
  29.  Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene.
FAIDA NYINGINEZO

KILISHE:
􀀃 Tangawizi ikichemshwa na maji na kuongezwa sukari hutoa kinywaji ambacho ni kitamu na chenye ladha nzuri sana. Baadhi ya watumiaji hupendelea kuongeza asali, vipande vya machungwa au limao ili kuweza kupata ladha nzuri zaidi. Vilevile hutumika katika utayarishwaji wa vinywaji vingine viwandani kama soda, chai, kahawa nakadhalika.
􀀃 Hutumika kama kiungo muhimu cha kuongeza ladha kwenye vyakula mbalimbali kama biskuti, mikate, keki, nyama na vingine vingi.

CHAI YA TANGAWIZI
CHAI YA TANGAWIZI


􀀃 Utomvu unaotokana na zao hili umeonekana kusaidia sana katika kuondosha maumivu ya sehemu mbalimbali za viungo vya binaadamu. Unapochua utomvu huu mara mbili kwa siku sehemu zenye maumivu huweza kuondosha maumivu mbalimbali haraka, kwa mfano maumivu ya misuli, magoti, maumivu ya kichwa nakadhalika.
􀀃 Hukinga na kutibu kuwashwa na kukereketwa koo (Sore throat) na ugonjwa wa mafua ya sehemu ya juu (Upper respiratory truck infection).
ô€€¥Tafiti mbalimbali ulimwenguni zimethibitisha  tangawizi kuwa na uwezo mkubwa katika kuondosha homa za kutapika na kizunguzungu (motion fever) kwa wasafiri wa vyombo mbalimbali baharini na nchi kavu.
Pia huondosha kichefuchefu na kutapika kwa akinamama wajawazito na hata kwa wagonjwa wanaofanyiwa operesheni. Inasadikika kijiko 1 cha tangawizi iliyosagwa kinatosha kumuondolea kichefuchefu na kutapika mgonjwa baada ya kufanyika operesheni.





SUPU YA TANGAWIZI
SUPU YA TANGAWIZI

ô€€ƒ Tangawizi pia imegundulika kupunguza kwa kiasi kikubwa lehemu katika mishipa ya damu na kuzuia damu kuganda katika mishipa hiyo, hivyo kuzuia kutokea madhara ya kuziba kwa mishipa ya damu jambo ambalo linazaweza kusababisha maradhi ya moyo na kupooza kwa viungo vya mwili.
􀀃 Tangawizi pia imegundulika kuwa dawa muhimu kupunguza au kuondosha kabisa maumivu wanawapata kinamama wengi wakati wa hedhi.
􀀃 Vilevile tangawizi imedhihirisha kuwa na uwezo mkubwa kuponya haraka maumivu makali ya tumbo yanayowapata mara kwa mara watoto wadogo.
􀀃 Katika baadhi ya nchi tangawizi inatumika katika kuhifadhi chakula kwa muda mrefu, hii inatokana na ukweli kwamba ina uwezo mkubwa wa kuua aina nyingi za bakteria kama vile E.coli, Salmonella na wengine wengi ambao huharibu vyakula vyetu.
􀀃 Tangawizi hukiamasisha kimengenyo mwilini kilichopo mwetu kiitwacho Gastric juice kufanya kazi ipasavyo na hivyo husaidia kuzalisha joto la mwili ambalo huwapa nafuu wagonjwa wengi wa mafua na maumivu ya tumbo.
􀀃 Watu wengi ulimwenguni hutumia mmea huu kama dawa ya kuondoa harufu mbaya kinywani.
􀀃 Hutumika katika utengenezaji wa siki (vinegar) ambayo huhamasisha hamu ya kula.

MFANO WA BIDHAA ZA TANGAWIZI
HITIMISHO
zingatia sana matumizi haya yatakusaidia , aksantee ufuatiliaje mwemaaa na karibu tena

Post a Comment

0 Comments